Posts

Chama kusimamishwa simba

Image
  Chama kusimamishwa simba Club ya Simba imetangaza kuwasimamisha kazi Wachezaji wake wawili Nasoro Kapama na Clotous Chota Chama kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu. Taarifa ya Simba imesema Wachezaji hao wawili pia wamepelekwa katika kamati ya nidhamu ya Simba SC kwa ajili ya hatua zaidi.  "Uongozi wa Club ya Simba unapenda kuwakumbusha Watumishi wake wote kuzingatia misingi ya maadili na nidhamu kwani haitosita kumchukulia hatua yeyote atakayethibitika kwenda kinyume na utaratibu huo"